google-site-verification: googleabbfd1327a3af7a3.html

Badili maisha yako sasa kwa kuwa na fikra sahihi.

Kujifunza zaidi juu ya maisha na mafanikio, nakualika kwenye kundi la whats app kujifunza kwa kina. Tututumie ujumbe kwa njia ya whats app kwenda 0687449428 kupata utaratibu wa kujiunga.

Nov 13, 2015

Kama Unaona Maisha Ni Magumu Utawezaje Kushinda?

No comments :
Hebu kaa chini na jaribu kujiuliza maswali haya kwa muda kidogo? Maisha yako ni nini? Una mtazamo gani unapofikiria juu ya maisha yako? Je, maisha yako yanakupa kile unachokihitaji? Haya ni maswali ambayo unapaswa kujiuliza ili yakupe dira,mwelekeo na picha ya maisha yako unavyotaka yawe.
Namna unavyoyaona maisha yako ndivyo unavyoyatengeneza. Namna ambavyo unaishi na malengo ndiyo yanaeleza maana ya maisha yako. Watu husema vitu tofauti kuhusu maisha kama vile maisha ni safari, maisha ni kitendawili kigumu, maisha ni kama duara, maisha ni kama foleni au maisha ni mchezo mchafu.
Lakini kila unapojiuliza wewe mwenyewe maisha ni nini! Unapata picha gani? Watu wengi wanaelewa maisha kupitia mavazi, vitu vya thamani, magari, mtindo na pesa au kwa namna nyingine kwa kadri jinsi wanavyoyatafsiri.
Picha uliyonayo juu ya maisha inakuhamasisha kwa hayo uliyonayo. Kama una picha ya maisha ni kama riadha utafanya mambo yako harakaharaka na kukazana. Kama una picha ya maisha ni mapambano utafanya chochote kupigania maisha yako. Ila kila siku upo katika mtihani au mchezo unaopaswa kushinda wala si kushindwa. Maisha ni jaribio la muda mfupi. Kwenda ngazi nyingine unahitaji kushinda mtihani kila siku.

KAMA UNAONA MAISHA NI MAGUMU UTAWEZAJE KUSHINDA?
WEWE NI MSHINDI WA MAISHA YAKO.
Maisha yamegawanyika katika ngazi tunazopaswa kuzivuka na kushinda. Huu ni ushindi wa lazima kwako, ambao ni lazima uushinde kama vile ulivyo mchezo wa mpira wa miguu. Sote tunapaswa kushinda maisha katika ngazi mbalimbali kama vile, ngazi ya makundi(Utoto), Robo fainali( Kijana),Nusu fainali(Mtu mzima) na fainali( Uzee).
Ili ushinde lazima uwe na kanuni, mbinu na mipango madhubuti ya kushinda. Kama vile kilivyo kikosi cha mpira wa miguu, tumia kikosi cha mambo yafuatayo kushinda katika maisha yako.
Kikosi cha kwanza cha mambo yako kitakachokupeleka kwenye mafanikio kiwe hiki:-
1. Kweli.
2. Utu wema.
3. Uvumilivu.
4. Uwajibikaji.
5. Imani.
6. Msamaha.
7. Elimu.
8. Furaha.
9. Umoja.
10. Kiasi
11. Upendo.

KAMA UNAONA MAISHA NI MAGUMU UTAWEZAJE KUSHINDA?
UKIWEKA JITIHADA NA KUVUMILIA UTASHINDA.
Kikosi cha ziada weka au fanya mambo haya:-
1. Uadilifu.
2. Haki na heshima.
3. Uaminifu.
4. Ndoto.
5. Fadhili.
6. Upole.
7. Uelewa.
Tambua wewe ndiye kiongozi na kocha wa maisha yako unatakiwa kuyasimamia na kuhakikisha unafanya mambo hayo ili kufanikiwa.
Unapokuwa na kikosi imara kama hicho ni rahisi kupambana na kikosi angamizi cha maisha yako kama magonjwa, umaskini, kufeli, marafiki wabaya, tamaa na kujidharau. TAMBUA USHINDI KWAKO NI LAZIMA kama utayaona maisha yako kwa mtazamo chanya.
Nikutakie siku njema, yafanyie kazi mambo hayo na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamsika.
Makala hii imeandikwa na Noel Ngowi wa Moshi- Tanzania. Kama una maoni au ushauri wasiliana na mwandishi wa makala hii kwa email truesuccess89@gmail.com



  


No comments :

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.